Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limemkamata Mchungaji Peter Msigwa    Mbunge wa Iringa Mjini  Peter Msigwa [CHADEMA] amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa jukwani akifanya mkutano wa hadhara  Jimboni kwake
    Mbunge huyo amekamatwa akiwa anahutubia wananchi wa kata ya Mlandege Jimboni humo  kwa mjibu wa taarifa zilizotufikia ghafla Jukwaa lilizungukwa na Asikali wa kutuliza Ghazia [FFU] na kumtaka kushuka jukwani .
     Msigwa alitii na kushuka na hatimaye moja kwa moja  Askali walimchukua na kumpeleka kituo cha Polisi cha Iringa Mjini.
     Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Julius Mjengi  amedhibitisha kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Iringa Mjini.na kusema taarifa zaidi ya kukamatwa kwake itatolewa baadaye.


  Imechapishwa na GEORGE MWITA

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post