Ludewa wapata neema ya kunufaika na huduma ya mawasiliano

  Ludewa waanza kufaidika na huduma ya mawasiliano
Wakazi wa eneo la mwambao wa ziwa Nyasa Wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe baada ya Kukaa bila mawasiliano ya Simu kwa miaka mingi tangu Kuumbwa kwa Dunia hatimaye wamepata matumaini baada ya Serikali kuanza ujenzi wa minara nane ya simu katika eneo hilo.
Wakizungumzia suala la ujenzi wa minara hiyo, baadhi ya madiwani wa Ukanda wa Ziwa Nyasa wamesema kuwa ujenzi wa mianara hiyo utakuwa ni utatuzi mkubwa wa suala la mawasiliano katika ukanda huo.
Madiwani hao wamevitaja Vijiji ambavyo Serikali inajenga Minara hiyo ya Simu kupitia Kampuni ya Halotel Kuwa ni Pamoja na Vijiji vya Nindi na Ntumbati katika kata ya Lupingu, Ndoa na Kimata kata ya Makonde, Kilondo na Nsele Kata ya Kilondo pamoja na Vijiji vya Lumbila na Nkanda katika Kata ya Lumbila ambapo Vijiji vya kata ya Lifuma Vitategemea Mawasiliano kutoka Vijiji Jirani.
Aidha, viongozi hao pamoja na Wananchi katika Mwambao wa Ziwa Nyasa wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea Kusikiliza Kero za wananchi wa Ludewa kupitia Mbunge wao, Deo Ngalawa na kuzitatua.
Hata hivyo, serikali Imetoa Pesa kwa ajili ya Kukarabati barabara ya kutoka Lumbila Kupitia Vijiji vya Kijombo wilayani Makete hadi Ludewa Mjini sambamba na Kuimarisha Huduma ya Afya kwa kukarabati vituo vya afya vya Mlangali, Makonde na Manda pamoja na Ujenzi wa Vituo Vipya vya Afya katika kila Kata.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post