lumbesa yaendelea kudhibitiwa na wakala wa vipimo.

wakala wa vipimo anaendelea kuimarisha matumizi sahihi ya vipimo katika maeneo mbalimbali hususani yanayohusu ufungashaji batili maarufu kama 'LUMBESA' dhumuni kubwa ni kumlinda mkulima.
              akizunguzumza mwishoni mwa wiki,  ofisa mtendaji Mkuu wa wakala wa vipimo  Dk ludovick manege  alisema jukumu kuu la wakala wa vipimo ni kuakikisha  vipimo vyote ni sahihi kwa mujibu wa sheria ya vipimo sura 340 ya mwaka 2002.
    amesema wanatekeleza sheria  hiyo, kama ilivyo fanyiwa mabadliko katika sheria ya mabadiliko ya sheria mbalimbali namba 3 ya 2016 kifungu cha 42(c) , 47, 48 na pia kifungu namba 4 kanuni za vipimo (ufungashaji wa bidhaa)
    katika kuelekea tanzania ya viwanda, Dk manege amesema jukumu lake ni kuhakikisha haki na usawa wa vipimo katika biashara na sehemu nyingine zinazo tumia vipimo zinakuwa sahihi kwaajili ya kuboresha maisha ya jamii.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post