Umoja wa madereva waendeshabajaji Makambako wamlalamikia Mzaburi.

 Umoja wa Madereva waendesha bajaji Makambako Mkoani Njombe umemlalamikia Mzaburi kwa kukiuka makubaliano waliokubaliano kupita katika kipande cha barabara ambachokilikataliwa na Mzaburi mara ya kwanza na baadae wakakubaliana kupita.

    Hayo yamesemwa na katibu wa umoja huo Agasto Shauri kwenye mkutano wa madereva waendesha bajaji pamoja na wamiliki wa bajaji uliofanyika katika uwanja  Amani Mjini Makambako Mkoani Njombe.
   Mkutano huo ulihudhuriwa na Mamia ya waendesha bajaji ambapo walitoa kero zao mbele ya Mgeni rasimi  Katibu wa Vijana CCM, Wilaya  ya Njombe bwana Daniel Muhanza.
  Viongozi hao wa bajaji walimlalamikia Mzaburi huyo kuwa wenda kuna mtu mwenye manufaa binafsi kulingana na Mzaburi huyo bwana Mdagasule aliefika kwa niaba ya Mkurugenzi wake  kukataa makubaliano waliofanya na viongozi wa Bajaji.
       Katibu wa Vijana wa CCM Wilaya ya Njombe ,aliyekuwa muarikwa Mgeni lasimi  amemtaka Mzaburi huyo kufika mwafaka na kukubaliana na madereva wapite kwenye kipande kilichokataliwa kama kulipa mapato ya sh, 500/= madereva wapotayari kulipa na siyo kuwanyanyasa kwa maana wapotayari kulipia ushuru  wa sh 500/= Ili wawezekupita.
       Kwa Mjibu wa Mzaburi amesema kuwa makubaliano yalikuwepo lakini hawakufika maamuzi ya mwisho kuwaruhusu kupita katika eneo hilo.
      Daniel Muhanza , Amempa Mzaburi huyo siku mbili ahakikishe wanafanya makubaliano na viongozi wa madereva bajaji la sivyo atachukua hatua nzito kuhusiana na mzaburi huyo.  Kwa upande wake Mzaburi huyo bwana Mdagasule amesema kuwa hawezikukubaliana na maamuzi aliyoyatoa bwana Daniel Mhanza na lasivyo wataandika barua kwenda kwa Mkurugenzi aliye wapa tenda hiyo.
     Nao baadhi ya Mdereva waliokuwepo wamesema kuwa wapotayari kulipa ushuru wa sh 500/=kwa siku ila wanachokiomba waruhusiwe kupita barabara ilyonzuri ili kunusuru kuharibika bajaji zao kila muda.
    Nao viongozi wa umoja wa waendesha Bajaji wametumia frusa hiyo ya Mkutano kuwaasa baadhi ya madereva ambao sio waminifu na wanaofanya vitendo vya kuwaibia abiria mizigo yao na kuna wengine ambao siyowaaminifu wanatumia mwanya wa uderava kuwatongoza wanawake na dereva atakayebainika atapata adhabu ikiwa nipamoja na kufungiwa kufanya kazi ya udereva katika mji wa Makambako Mkoani Njombe.
     Pia Viongozi wa umoja wa waendesha bajaji wameshauriwa madereva hao kuwa  na mshikamano pindi wanapokuwa wanapata matatizo.
     Kwa mjibu wa Madereva bodaboda wamesema kuwa kuna madereva wachache  ambao siyo waminifu wanawarubuni wanawake kwa kuwatongoza na kuiba baadhi ya mizigo ya abiria na kushauri kuwa dereva atakaye jihusisha na vitendo viofu achukuliwa hatua   kali ili kukomesha vitendo hivyo na kazi ya Dereva iheshimiwe kama kazi nyingine.

                             

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post