Maandamano sudani yasababisha shule kufungwa

            Kutokana na maandamano yaliyoibuka baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano katika Jimbo la  Kordofani Mamlaka ya utawala wa Kijeshi  nchini Sudani imeamuru  masomo kusimamishwa na shule kufungwa  nchi nzima.

        Pia maandamano hayo yalilenga katika malalamiko kwenye sekta ya mafuta  na upungufu wa mkate ikiwa wanafunzi wanne  na mwananchi mmoja wameripotiwa kupoteza maisha ,watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya risasi kufyatuliwa kiholela.
        Kutokana na taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Suna  mamia ya wanafunzi waliovalia sare za shule waliandamana  wakiwa wanapunga bendera za Nchi yao kudai haki ya wenzao waliouawa na kupelekea mamlaka kuamuru Magavana wa Majimbo yote kufunga shule zote mpaka yatakapotolewa maelezo mengine.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post