Waziri Lugola awaka moto.

Waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugola amesema kuwa mpango wa Serikali ni kukemea vikali biashara  haramu ya usafirishwaji binadam inayofanyika na baadhi ya wafanya biashara kwa dhumuni la kujipatia kipato .
Amesema hayo Jijin Dar es salaam,wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kudhibiti biashara  ya binadam, ambapo amesema biashara hiyo kwa sasa ni sawa na biashara ya utumwa.


    '' Biashara haramu ya usafirishaji wa  binadam inayoongoza hapa nchini ni  ya kutoka mkoa mmoja kwenda  mkoa mwingine  ambapo waathirika  zaidi  ni watoto wadogo,wasichana na vijana ambao umri wao ni miaka 13 hadi 24 hali hii  inadhihirisha  wazi kwamba kuna utumwa licha ya utumwa ambao  tulifanyiwa  na wenzetu wakati ule, bado kuna baadhi  yetu  wanaowafanya  watanzania wenzetu  kuwa  watumwa.''Amesema Kangi Lugola.                                                                                      Ikumbukwe kuwa siku ya kupinga biashara ya binadamu kimataifa huadhimishwa  kila mwaka julai 30.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post