Tembo 55 wamekufa njaa katika mbuga ya kitaifa ya Hwange, nchini Zimbabwe.

    Nchini Zimbabwe Tembo Taklibani ya 55 wafa njaa kutokana na kukubwa kwa ukame ulikokithiri katika muda wa miezi miwili katika Mbuga ya Kitaifa ya Hwaange nchini humo.
  Akizungumza msemaji wa Mbuga hiyo Tinashe Farawo amesema kuwa''Hali mbaya'',''Tembo wanakufa kutokana na ukame na hili ni tatizo kubwa''.
   Kutokana na kiwango kikubwa cha ukame Nchini Zimbabwe imeepelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha mimea nchini humo.    Ambapo theluthi moja ya watu nchini humo wameripotiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula wakati mgogoro wa kiuchumi ukiendelea nchini humo.
Mwezi Agosti, ripoti ya Shirika la Chakula Duniani ilisema kuwa watu milioni mbili wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.
Baadhi ya tembo walipatikana katika eneo la mita 50 (yadi) ya maji -kuashiria kuwa walitembea mwendo mrefu bila maji na hatimaye kufa muda mfupi kabla ya kuyafikia.
Tembo hao wamesababisha "uharibifu mkubwa" wa mimea katika mbuga ya Hwange, Bw. Farawo alisema.
Mbuga hiyo inawahifadhi karibu tembo 15,000 lakini kwa sasa kuna zaidi ya tembo 50,000.
   Lakini pia,Bwana Farawo aliongeza kwa kusema kwamba mbuga hiyo imejitaidi kufanya jitihada binafsi pasipo kupokea ufadhili kutoka Serikalini kama vili kuchimba visima lakini imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa fedha kwa ajili ya kuendelea na mradi huo.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post