Halima Mdee ashinda Uenyekiti BAWACHA

        Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) baada ya kupigiwa kura 317 za ndio.
Katika uchaguzi huo ulioanza jana Alhamisi Desemba 12,2019 na kumalizika leo Ijumaa Desemba 13, 2019 Mdee alikuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya uwenyekiti .
Msimamizi wa uchaguzi huo, Sylvester Masinde amemtangaza Mdee kushinda kwa mara nyingine huku Hawa Mwaifunga akichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa baraza hilo.
    Masinde amesema Mwaifunga ambaye ni mbunge wa viti maalumu amepata kura 220 akiwashinda Aisha Luja, Marceline Stanslaus na Mary Nyagabona.
“Makamu mwenyekiti Zanzibar ni Sharifa Suleiman aliyepata kura 184 dhidi ya Mariam Msabaha aliyepata kura 120. Uchaguzi wa makamu mwenyekiti Zanzibar ulirudiwa baada ya awamu ya kwanza wagombea kushindwa kufikisha asilimia 50 ya kura,” amesema Masinde.
Leo mchana unaendelea uchaguzi wa katibu mkuu wa baraza hilo na naibu wawili wa Bara na Zanzibar kukamilisha safu ya uongozi ya Bawacha.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post