Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika ataja vipaumbele

     Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema moja ya kazi yake kubwa kwenye chama hicho ni kukiandaa kuelekea kushinda na Uchaguzi Mkuu wa 2020.
       Mnyika ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo moja ya majukumu yake makubwa ni kukiandaa chama hicho kuelekea kushinda dola.
  "Kazi yangu na kiongoza chana Makao Makuu kwenda kuchukua dola, na katika kutekeleza hili kwanza tuna vipaumbele vitano cha kwanza ni tume huru ya Uchaguzi,"Amesema Mnyika
   Amesema vipaumbele hivyo ni kudai tume huru ya uchaguzi, maandalizi ya wagombea kuelekea uchaguzi mkuu, ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuendeleza sera ya Chadema msingi na  Chadema Digital.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post