Mtu mmoja auawa kwa kupingwa na nyundo

       Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Sosteni Myamba (44) mkazi wa kijiji cha Itipingi halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe inasemekana ameuawa kwa kupigwa nyundo kwa madai ni kutokana na imani za kishirikina.Mwenyekiti wa kijiji cha Itipingi Ayubu Mgeni amethibitisha hilo na kufafanua kuwa marehemu huyo alikuwa na tabia ya kuwatuhumu baadhi ya ndugu akiwemo baba yake mzazi kuwa ni mshirikina hali ambayo imepelekea kuibuka kwa mgogoro ndani ya familia hiyo.
Kiongozi wa familia hiyo Aidani Myamba amesema marehemu  alikuwa ana matatizo ya akili hali ambayo ilimfanya awe mtu wa kutuhumu wengine kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina.Hata hivyo Jacob Myamba ambaye ni mdogo wa marehemu huyo anashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya kipolisi makambako kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post