Shirika la Hifadhi za Taifa{TANAPA} limezindua kampeni maalumu ijulikanyo kwe jina la ‘’Talii na TANAPA

Shirika la Hifadhi za Taifa{TANAPA} limezindua kampeni maalumu ijulikanyo kwe jina la ‘’Talii na TANAPA msimu huu wa sikukuu ya X mass na Mwaka mpya’’ kwa kushirikisha wasanii maarufu,warembo ,watangazaji maarufu na watu maarufu lengo ni kutaka kuhamashisha watanzania kutembele hifadhi za Taifa badala ya kwenda kutalii nje ya nchi katika kipindi hicho.
Hayo yalisemwa na Kaimu Kamishina wa Uhifadhi wa TANAPA,Witness Shoo mbele ya waandishi wa habari kwa kushirikisha viongozi mbalimba wa uhifadhi,wasanii na watangazaji tukio lililofanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Arusha..

IMG-20191214-WA0109
Shoo alisema kuwa lengo la TANAPA ni kutaka kila mtanzania kuwa mzalendo na nchini yake kwa kutembelea vivutio vilivyokuwa katika hifadhi 22 hapa nchini kwa kuvitembelea na kuwa balozi wakubwa wa kuvitangaza.

Alisema kundi la kwanza la wasani,watangazaji na watu maarufu litaanza kufanya kampeni hiyo desemba 20 mwaka huu katika hifadhi sita ikiwemo Ruaha,Katavi,Mkomazi,Rubondo,Mikumi na hifadhi ya Gombe iliyopo Mkoani Kigoma.

Kamishina huyo alisema katika Hifadhi ya Ruaha msanii Idrisa Sultan atakwenda kutalii katika mbuga hiyo na kuitangaza ndani na nje ya nchi katika mitandao ya kijamii kwani anawafuasi wengi katika mitandao ya kijamii hivyo anawajibu wa kutoa ujumbe kwa watanzania kuacha kukimbilia nje ya nchi kutalii badala yake watembelee hifadhi Taifa.

Alisema msanii Mrisho Mpoto atakuwa katika Hifadhi ya Katavi,mrembo wa mwaka Nancy Sumary atakuwa katika hifadhi ya Mkomazi,mtangazaji kijana aliyejipatia umaarufu hapa nchini,Milard Ayo na Miss wa mwaka 2018 Elizaberth Makune watakuwa na jukumu la kuwakumbusha watanzania kutembelea hifadhi ya Robondo.

Wengine ni pamoja na wasanii wa muziki wa Bongo flava Lulu Abas maarufu kwa jina la Lulu Diva atakuwa katika Hifadhi ya Mikumi na msani aliyetambulika kwa jina moja la Rubby atakuwa katika hifadhi ya Gombe.

Naye Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwataka watanzania kuwa na tabia ya kutembelea mbuga za wanyama katika vipindi vyote vya sikukuu ya X Mass na Mwaka mpya na sikukuu nyingine kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha na pia kuvitangaza vivutio hivyo kwa faida ya nchi.

Shelutete alisema kuwa wasanii wa fani mbalimbali,watu maarufu na watangazaji watashirikishwa katika kampeni hiyo iliyolenga kumtaka mtanzania kupenda cha nchi yake na kuacha kujali vya nje .

Naye Msanii Idrisa Sultan alisema kuwa katika maisha yake hajawahi kufika katika hifadhi ya Ruaha hivyo kwa fursa aliyopewa atahakikisha anaitangaza hifadhi hiyo kwa kadri awezavyo lengo ni kutaka watanzania kuwa wazalendo na kupenda cha kwao na kuacha ulimbukeni wa kikumbilia nje ya nchi kama Dubai na kungine kwa kutumia mamilionin ya pesa bila ya sababu za msingi.
Kaimu Kamishina wa Uhifadhi wa TANAPA,Witness Shoo akizindua rasmi  kampeni ya Talii na TANAPA , ambayo mabalozi wake ni baadhi ya wasanii pamoja na watangazaji ndani ya ukumbi Wa ofisi za makao makuu ya shirika hilo.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post