Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2020 Mkoa Wa Njombe


Mkoa wa Njombe umetangaza kuto achwa mwanafunzi yeyote wa darasa la saba aliyefaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 kutokana na uwepo wa miundombinu ya kutosha,pamoja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wazazi na walezi watakao shindwa kuwafikisha wanafunzi shuleni.

Katibu tawala mkoa wa Njombe Katarina Revocati ameyasema hayo katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi watakao jiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo .

“Malengo ya kikao hiki ni kutangaza rasmi matokeo ya wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi kwa mwaka 2019 lakini la pili ni kutangaza idadi ya wanafuzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2020 na natangaza rasmi wanafunzi wote waliofaulu watakwenda kidato cha kwanza na tunaomba sana idadi itakayoenda kuanza kidato cha kwanza  miaka minne ijayo tutakapo kuwa kwenye kikao kama hiki tuwe na idadi hiyo hiyo itakayokuwa inahitimu”Alisema Katarina Revocati
Awali afisa elimu mkoa wa Njombe mwalimu Gift Kyando alisema mwaka 2019 watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 18,249 na waliofaulu kwa kupata alama 100-250 ni 15,768 sawa na asilimia 86.4

Aidha Kyando amesema kwa ujumla matokeo ni mazuri kwasababu mkoa bado upo katika ushindi wa wastani daraja “A” na mkoa kitaifa umeshika nafasi ya 9 kati mikoa 26 na mwaka 2018 mkoa ulishika nafasi ya 10 kati ya mikoa 26

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri amesema matokeo hayo ni kazi nzuri na matokeo ya mpango wa serikali ya awamu ya tano hivyo kwa sasa kazi waliyonayo ni kuendelea kusimamia kuhakikisha swala la miundombinu kutokuwa changamoto.


==>>Bonyeza Hapo Chini Kuona Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mkoa wa NJOMBE   Pamoja na Mikoa Mingine. 

<<BOFYA HAPA  KUTAZAMA MAJINA YOTE>>

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post