Malema amuita Odinga wamuunge mkono Ruto

Kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), cha Afrika Kusini, Julius Malema, anasema amezungumza kwa njia ya simu na Rais mteule wa Kenya William Ruto na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa Taifa hilo la Kenya huku akisema anamuunga mkono.
Katika hotuba yake kwa umma wa Afrika Kusini Agosti 23, 2022, Malema amesema alitoa wito wa kumpongeza Ruto kwa kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kuwa mshindi wa uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022.
Amesema, katika maongezi yake alimtaka mgombea Urais wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga, kukubali matokeo na kumuunga mkono Ruto, ili kuweza kuijenga Ke“Ruto lazima awe sehemu ya juhudi za kujenga bara huru ambalo halina vita na umaskini,” alisema Mkuu huyo wa EFF katika kongamano ambalo chama chake kinashughulikia masuala kadhaa ya kitaifa kwa kulihusisha bara la Afrika.
Awali, akisoma taarifa ya chama hicho, Malema aliwapongeza Wakenya kwa kuendesha uchaguzi wa amani ambao ulikamilika kwa William Ruto kutangazwa mshindi dhidi ya mpinzani wake, Raila Odinga.
Madai ya Malema, yanakuja huku ikiwa tayari Raila Odinga ameshawasilisha pingamizi lake Mahakama ya Juu ya Kenya kupinga tangazo la IEBC lililomuidhinisha Ruto kama Rais mteule wa Jamhuri ya watu wa Kenya.nya na kudumisha Demokrasia


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post