Mzee adai kuibiwa Uniti 196 za Umeme Ludewa Mkoani Njombe

 


Mzee Nuru Kahiza ambaye ni muuguzi mstaafu mkazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,ameiomba serikali kupitia mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga kumrudishia UNIT  196 za umeme zilizopotea wakati shirika la umeme Tanzania (TANESCO) lilipokuwa likimbadilishia mita ya umeme.
Mzee Kahiza amesema amezulumiwa kiasi hicho cha UNIT wakati akiwa amesafiri huku akiwa amemuachia binti yake kazi ya kuandika idadi ya UNIT zilizokuwa zimebaki kwenye mita kabla ya kubadirishiwa lakini hata hivyo licha ya kufuatilia swala lake amekuwa akizungushwa na wataalamu kutoka TANESCO.
“Wamenizulumu UNIT zangu,wakati wakiwa wanabadirisha mita mimi nilikuwa nimesafiri nikamuagiza binti yangu uandike idadi ya UNIT nilizonazo karibu 196,nimeenda kwao mara nyingi hawanijibu wanasema oooo makao maku mapka leo hawajanilipa UNIT zangu kwa hiyo wametuzulumu wanagapi?”alisema Kahiza
Mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga ameahidi kushughulikia changamoto hiyo na kumuomba mzee Kahiza kuwa mvumilivu kwa kuwa sasa changamoto imefika mikononi mwake huku akimuahidi kuongozana naye katika ofisi za shirika la umeme (TANESCO) wilaya ya Ludewa ili kupata muafaka juu madai yake ikiwemo pia kuondolewa kwa nyaya za umeme zilizopita  juu ya paa lake la nyumba

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post