Watu 10 wameuwawa Afghanistan

 

Watu wasiopungua 10 wameuwawa kufuatia mripuko wa bomu uliotokea ndani ya msikiti mmoja katikati mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul wakati wa ibada ya jioni jana Jumatano. 
Kulingana na shuhuda mmoja aliyezungumza na shirika la habari la Associated Press mshambuliaji wa kujitoa muhanga alijiripua kwenye msikiti wa Siddiquiya mkasa uliosababisha vifo hivyo vya watu 10 na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.Miongoni mwa waliouwawa ni pamoja na kiongozi mashuhuri wa kidini katika eneo hilo, Amir Mohammad Kabuli.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo ambalo ni la hivi karibuni kabisa kutokea nchini Afghanistan iliyotimiza mwaka mmoja chini ya utawala wa Taliban. Wapiganaji wenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu wamezidisha mashambulizi yao wakiwalenga Taliban na rais tangu wanamgambo hao walipotwaa madaraka Agosti mwaka jana

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post