Mbunge wa Tarime Mjini ameishukuru Serikali kwa kutoa shiling Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa Soko

 Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki amepongeza serikali ya awamu ya Sita ya Samia Suluhu Hassani kwa kutoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya uejnzi wa soko kuu na kusema kuwa ujenzi ukikamilika wa soko hilo wafanyabiashara wataondokana na kero ya kufanyiabiashara maeneo yasiyo rasimi.

Kembaki alisema hayo juzi mbele ya Waziri wa Fedha na mipango Mwigulu Nchemba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya viwanja vya Tarafa mji ndogo wa Sirari mpakani mwa nchi jirani ya Kenya.

“Napenda kutumia nafasi hii kushukuru Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassani kwa kutupatia shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa soko kuu na wafanyabiashara wakapata maeneo rasimi ya kufanyia biashara na ukitoka hapa nakuomba ukapite mjini Tarime ukajionee kazi ambayo fedha hiyo inatekeleza”alisema Kembaki.

Mbunge huyo aliongeza kuwa wananchi wake wanafanya biashara katika mazingira magumu hususani wafanyabiashara wadogo ambao wanachukua bidhaa kutoka nchi jirani ya Kenya wanakamatwa hata kama watakutwa wanadumu moja la mafuta ya kula vinginevyo sharia rafiki itungwe kuwalinda wafanyabiashara kama hao.


  Kwa  mjibu wa  Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa Mara,Samweli Keboye (maarufu namkba Tatu) alisema kuna baadhi ya viongozi ambao sio waaminifu ambao wanafanya kazi kinyume cha sharia na kwa hali hiyo wanatengenezea mazingira magumu chama chake wakati wa uchaguzi ukifika.

Keboye aliomba serikali kuwachukulia hatua wale wote ambao watakuwa wanabainika wanafanya kazi kinyume cha sharia huku wakifanya kazi bila kuzingatia maadili na kuharibu sifa na heshima ya Chama chake cha CCM.

Katika mkutano huo Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba alisema serikali iliyopo inawajali watu wake na kuwa inajitahidi kuwatengenezea mazingira mazuri watu wake na wafanyabiashara kwa ujumla ili kuwaletea  maendeleo.

Waziri huyo aliwataka wananchi na viongozi kujenga nidhamu ya kazi ikiwemo kuheshimu sharia zilizopo pamoja na ile ya makusanyo ya kodi toka TRA kwa sababu ipo kwa mjibu wa sharia na kama kuna sharia iliyo onekene kuwa na ukakasi kuna haja ikarudi Bungeni kujadiliwa upya na kupitishwa ili kfanya kazi  siovinginevyo.

Mwigulu aliongeza kusema kuna haja Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kwa kushirikiana na halmashauri kutoa elimu kwa jamii juu ya bidhaa zinazolipiwa ushuru na kutozwa kodi na zile ambazo hazitozwi kodi ili wananchi wakae wakijua na kuondoa mgongano uliopo.

Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wale wote ambao wanajihusisha na kufanya biashara za mpakani kuondokana na swala zima la kukwepa kodi badala yake watii sheria kwa kulipa kodi sitahiki ili kujenga Taifa lenye umoja na usitawi


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post