Mlinzi Jeneza la Malkia aanguka ghafla

 Mlinzi anayelinda jeneza la Hayati Malkia Elizabeth II, ameanguka ghafla wakati wa maandalizi ya kuagwa kwa mwili wa Kiongozi huyo aliyeitawala Uingereza kwa muda mrefu (miaka 70), kwenye ukumbi wa Westminster Hall jijini London.

Tukio hilo, limetokea wakati raia wa Uingereza wakiendelea na zoezi la kuaga mwili wa Malkia huyo aliyefariki hivi karibuni, ambapo chanzo cha kuanguka kwa mlinzi huyo hakikuweza kufahamika mara moja.


Mara baada ya kuanguka kwa mlinzi huyo, Televisheni ambayo ilikuwa ikirusha matangazo hayo mubashara ilisitisha matangazo wakati mlinzi huyo akipatiwa matibabu ya dharura.

Jeneza la Hayati Malkia Elizabeth II, linalindwa kikosi maalum kinachofahamika kama Sovereign’s Bodyguard.Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post