Naibu Gavana afariki akiwa ndani ya Ndege : Kenya

 Gavana wa Kaunti ya Baringo, Benjamin Cheboi amethibitisha kufo cha Naibu Gavana wa Kaunti ya Baringo nchini Kenya, Charles Kipng’ok amabye amefariki dunia muda mfupi kabla ya ndege kupaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kuelekea Mombasa.

Kipng’ok amefariki dunia ndani ya ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways, ambapo alitarajiwa kuungana na wakuu wengine wa kaunti kwa ajili ya kujitambulisha kwa Baraza la Gavana.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la ndege la  Kenya Airways imesema abiria huyo alitangazwa kuwa amefariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) huku ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Mombasa ikiwa bado ardhini.

“Kenya Airways PLC inasikitika kutangaza abiria wake alipata matatizo ya kupumua jioni hii alipokuwa akipanda KQ612, kuwa amefariki wakati wafanyikazi wa matibabu wa JKIA wakati ndege ikiwa chini,” imesema taarifa ya KQ.

Shirika hilo mapema mwezi huu lilithibitisha kwamba abiria aliyekuwa kwenye mojawapo ya safari zake za ndege kuelekea New York nchini Marekani kutoka Nairobi alifariki dunia, ikiwa ni tukio la pili kama hilo kuripotiwa katika muda wa siku tisa.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post