Sakata la Panya Road latua Bungeni

 

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, ameiagiza serikali kuchukua hatua za haraka kushughulikia vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na vikundi vya kama Panya Road.

Spika Dkt. Tulia ametoa maagizo hayo leo Septemba 15, wakati wa kikao cha Bunge kufuatia hoja ya dharura iliyowasilishwa na Mbunge wa Viti Maalum, Bahati Ndigo aliyeomba shughuli za bunge ziahirishwe kwa muda kujadili kuhusu usalama wa raia na kuongezeka kwa vitendo hivyo vinavyoathiri maisha ya watu.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post