Jumuiya ya Wanawake [UWT} Wilaya ya Wanging'ombe ya panda miti kusaidia utunzaji wa mazingiraNa Mwandishi  George Mwita - Njombe 

Jumuiya ya wanawake UWT wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe imeunga mkono jitihada za serikali kupitia Wizara ya mali asili na utalii kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupanda miti ili kusaidia utunzaji wa mazingira na kutoa wito kwa jamii kuendelea kupanda miti ili kuhifadhi mazingira yao.
Katibu wa Jumuiya hiyo Mary Rashid akiwa na baadhi ya wajumbe katika zoezi Hilo amesema.
"UWT Wanging'ombe leo katika kuelekea kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) tumefanikiwa kugawa kadi za uanachama kwa wanachama wapya 70 wa UWT na kupanda miti kwenye shamba letu lenye ukubwa wa ekari 1"alisema Mary Rashid 
Pia ameongeza kuwa"Tunapanda miti kama kitega uchumi cha Jumuiya yetu hapo baadaye itakapokomaa licha ya kuwa shabaha yetu nyingine ni kuendeleza utunzanji wa mazingira na kufanya wilaya yetu kuwa na mvua za mara kwa mara"Mary Rashid Katibu UWT wilaya ya Wanging'ombe

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post