Mwalimu aliyeonekana katika Video akimchapa mwanafunzi kwenye nyayo za Miguu na kumkanyaga achukuliwa hatua za kusimamishwa kazi
Mwalimu akimchapa mwanafunzi

Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Mwalimu anayeonekana kwenye video fupi inayosambaa mitandaoni akimchapa mwanafunzi kwenye nyayo za miguu yake huku amemkanyaga tayari amekwishachukuliwa hatua za kusimamishwa kazi.


Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Mwalimu huyo ni wa shule ya msingi iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera na tukio hilo limetokea Januari 10, 2023.

Aidha waziri Dkt Gwajima akatoa rai kwa Walimu, "Waalimu zingatieni utaratibu wa adhabu kwa wanafunzi, lazima sheria ziheshimiwe,".

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post