Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kurejea Nchini 01Machi 2023

Hatimaye Tarehe ya Godbless Lema Kurudi Tanzania Yatanjwa, Wananchi Kumpokea

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema, atarejea nchini March 01, 2023, siku ya Jumatano, saa sita kamili mchana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

“Lema, aliondoka nchini na kuelekea Kenya tarehe 8 November 2020 ambako alikaa kwa mwezi mmoia na kisha tarehe 8 December 2020 alielekea nchini Canada ambako alipata hifadhi ya kisiasa kutokana na kuwepo kwa tishio la kuuawa yeye na Familia yake”

“Atakaporejea nchini, Lema atapokelewa uwanja wa ndege (KIA) na Viongozi wa Chama, Wananchama na Wananchi watakaojitokeza kumpokea na kisha atakwenda moja kwa moja kwenye mkutano wa hadhara utakao fanyika Arusha Mjini”

“Lema, baada ya kurejea atakuwa na vikao ya kazi ya kuongoza kikao cha Kamati ya Utendaji ya Kanda na Baraza la Uongozi la Kanda ya Kaskazini na kisha ziara za mikutano ya hadhara na vikao vya ndani kwenye Mikoa yote ya kanda ya Kaskazini (Tanga, Kllimanjaro, Arusha a Manyara), pia atashiriki kwenye mkutano Mkuu wa Jimbo la Arusha Mjini na atakuwa na ratiba ya ziara kwenye Kata mbalimbali za Jimbo la Arusha Mjini” 
Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post